Mathayo 11:4 - Swahili Revised Union Version Yesu akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie Yohane mambo mnayoyasikia na kuyaona: Biblia Habari Njema - BHND Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie Yohane mambo mnayoyasikia na kuyaona: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie Yohane mambo mnayoyasikia na kuyaona: Neno: Bibilia Takatifu Isa akajibu, “Rudini mkamwambie Yahya yale mnayosikia na kuyaona: Neno: Maandiko Matakatifu Isa akajibu, “Rudini mkamwambie Yahya yale mnayosikia na kuyaona: BIBLIA KISWAHILI Yesu akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona; |
vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema.
Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya;
Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika.
Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.
Lakini ushuhuda nilio nao mimi ni mkuu kuliko ule wa Yohana; kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba ili nizimalize, kazi hizo zenyewe ninazozitenda, zanishuhudia ya kwamba Baba amenituma.