Mathayo 10:12 - Swahili Revised Union Version Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mnapoingia nyumbani wasalimuni wenyeji wake. Biblia Habari Njema - BHND Mnapoingia nyumbani wasalimuni wenyeji wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mnapoingia nyumbani wasalimuni wenyeji wake. Neno: Bibilia Takatifu Mkiingia kwenye nyumba, itakieni amani. Neno: Maandiko Matakatifu Mkiingia kwenye nyumba, itakieni amani. BIBLIA KISWAHILI Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni. |
Nao, iwe watasikia au hawataki kusikia, (maana ndio nyumba ya kuasi hao), hata hivyo watajua ya kuwa nabii amekuwako miongoni mwao.
Na mji wowote au kijiji chochote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hadi mtakapotoka.
Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.
Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri Habari Njema ya amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote),
Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.
na hivi ndivyo mtakavyomwambia huyu aishiye salama, Amani na iwe kwako, na amani nyumbani mwako, na amani kwao wote ulio nao.