Mathayo 1:16 - Swahili Revised Union Version Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yakobo alimzaa Yosefu, mumewe Maria mama yake Yesu aitwaye Kristo. Biblia Habari Njema - BHND Yakobo alimzaa Yosefu, mumewe Maria mama yake Yesu aitwaye Kristo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yakobo alimzaa Yosefu, mumewe Maria mama yake Yesu aitwaye Kristo. Neno: Bibilia Takatifu naye Yakobo akamzaa Yusufu, aliyekuwa mumewe Mariamu, mama yake Isa, aitwaye Al-Masihi. Neno: Maandiko Matakatifu naye Yakobo akamzaa Yusufu ambaye alikuwa mumewe Mariamu, mama yake Isa, aitwaye Al-Masihi. BIBLIA KISWAHILI Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo. |
Ndipo alipowakataza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu yeyote ya kwamba yeye ndiye Kristo.
Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hadi nitakapokuambia; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.
Basi walipokutanika, Pilato akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi? Yule Baraba, au Yesu aitwaye Kristo?
Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na dada zake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake.
kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa ukoo wa Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.
Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.
akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa na umri wa miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,
Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu?
Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.