Nanyi mtamwarifu baba yangu habari za fahari yangu yote katika Misri, na za vyote mlivyoviona; mkafanye haraka kumleta huku baba yangu.
Matendo 7:14 - Swahili Revised Union Version Yusufu akatuma watu akamwita Yakobo babaye na jamaa zake wote pia, watu sabini na watano. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yosefu alituma ujumbe kwa baba yake na jamaa yote, jumla watu sabini na watano, waje Misri. Biblia Habari Njema - BHND Yosefu alituma ujumbe kwa baba yake na jamaa yote, jumla watu sabini na watano, waje Misri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yosefu alituma ujumbe kwa baba yake na jamaa yote, jumla watu sabini na watano, waje Misri. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Yusufu akawatuma kumleta Yakobo baba yake pamoja na jamaa yake yote; kwa jumla walikuwa watu sabini na watano. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Yusufu akawatuma kumleta Yakobo baba yake pamoja na jamaa yake yote, jumla yao walikuwa watu sabini na watano. BIBLIA KISWAHILI Yusufu akatuma watu akamwita Yakobo babaye na jamaa zake wote pia, watu sabini na watano. |
Nanyi mtamwarifu baba yangu habari za fahari yangu yote katika Misri, na za vyote mlivyoviona; mkafanye haraka kumleta huku baba yangu.
Na wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela, na Peresi, na Zera; lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani. Na wana wa Peresi, ni Hesroni, na Hamuli.
Na wale watu wote waliotokana na uzao wa Yakobo walikuwa watu sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo.
Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapatao elfu tatu.
Baba zako walienda Misri wakiwa watu sabini; na sasa BWANA, Mungu wako, amekufanya kama nyota za mbinguni kwa wingi.