Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake.
Matendo 4:22 - Swahili Revised Union Version maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arubaini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huyo mtu aliyeponywa alikuwa na umri wa miaka zaidi ya arubaini. Biblia Habari Njema - BHND Huyo mtu aliyeponywa alikuwa na umri wa miaka zaidi ya arubaini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huyo mtu aliyeponywa alikuwa na umri wa miaka zaidi ya arubaini. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa umri wa yule mtu aliyekuwa ameponywa kwa muujiza ulikuwa zaidi ya miaka arobaini. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa umri wa yule mtu aliyekuwa ameponywa kwa muujiza ulikuwa zaidi ya miaka arobaini. BIBLIA KISWAHILI maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arobaini. |
Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake.
Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa.
Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu.
Nao walipokwisha kuwatisha tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu; kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka;
Hata walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha habari ya mambo yote waliyoambiwa na wakuu wa makuhani na wazee.
Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea, mtu huyo alikuwa amelala kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza.