Akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.
Matendo 3:4 - Swahili Revised Union Version Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Petro na Yohane walimkodolea macho, naye Petro akamwambia, “Tutazame!” Biblia Habari Njema - BHND Petro na Yohane walimkodolea macho, naye Petro akamwambia, “Tutazame!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Petro na Yohane walimkodolea macho, naye Petro akamwambia, “Tutazame!” Neno: Bibilia Takatifu Wakamkazia macho, kisha Petro akamwambia, “Tutazame sisi.” Neno: Maandiko Matakatifu Wakamkazia macho, kisha Petro akamwambia, “Tutazame sisi.” BIBLIA KISWAHILI Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. |
Akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.
Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa katika hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
Akamkodolea macho, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Nikakitazama sana, nikifikiri, nikaona wanyama wa nchi wenye miguu minne, na wanyama wa mwituni, wale watambaao, na ndege wa angani.
Basi alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililoitwa tao la Sulemani, wakishangaa sana.
Wakati Petro alipoyaona haya akawajibu wale watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utauwa wetu sisi?