Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa bado mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu.
Matendo 21:6 - Swahili Revised Union Version na baada ya kuagana tukapanda melini, nao wakarudi kwao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha tuliagana; sisi tukapanda meli, nao wakarudi makwao. Biblia Habari Njema - BHND Kisha tuliagana; sisi tukapanda meli, nao wakarudi makwao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha tuliagana; sisi tukapanda meli, nao wakarudi makwao. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya kuagana, tukapanda kwenye meli, nao wakarudi manyumbani mwao. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya kuagana, tukapanda melini, nao wakarudi majumbani mwao. BIBLIA KISWAHILI na baada ya kuagana tukapanda melini, nao wakarudi kwao. |
Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa bado mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu.
Tazama, saa inakuja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; lakini mimi siko peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.
Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.
sikuona raha nafsini mwangu, kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali niliagana nao, nikaondoka kwenda Makedonia.