Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.
Matendo 2:21 - Swahili Revised Union Version Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo, yeyote atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.’ Biblia Habari Njema - BHND Hapo, yeyote atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo, yeyote atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.’ Neno: Bibilia Takatifu Na kila mtu atakayeliitia jina la Mwenyezi Mungu, ataokolewa.’ Neno: Maandiko Matakatifu Na kila mtu atakayeliitia jina la Bwana Mwenyezi Mungu, ataokolewa.’ BIBLIA KISWAHILI Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa. |
Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.
Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la BWANA ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama BWANA alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao BWANA.
Basi, nendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri.
Bwana akamwambia, Simama, nenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;
Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.
kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.
Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.