Petro akajibu, akamwambia Yesu, Rabi, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya.
Marko 9:6 - Swahili Revised Union Version Maana, hakujua la kunena, kwa kuwa waliingiwa na hofu nyingi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye na wenzake waliogopa hata hakujua la kusema. Biblia Habari Njema - BHND Yeye na wenzake waliogopa hata hakujua la kusema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye na wenzake waliogopa hata hakujua la kusema. Neno: Bibilia Takatifu Petro hakujua aseme nini kwa maana yeye na wenzake walikuwa wameogopa sana. Neno: Maandiko Matakatifu Petro hakujua aseme nini kwa maana yeye na wenzake walikuwa wameogopa sana. BIBLIA KISWAHILI Maana, hakujua la kunena, kwa kuwa waliingiwa na hofu nyingi. |
Petro akajibu, akamwambia Yesu, Rabi, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya.
Kisha likatokea wingu, likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye.
Ikawa hao walipokuwa wakijitenga naye, Petro alimwambia Yesu, Bwana mkubwa, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu; kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya; hali hajui asemalo.
Nami nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,