Marko 9:4 - Swahili Revised Union Version Wakatokewa na Eliya pamoja na Musa, nao walikuwa wakizungumza na Yesu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Elia na Mose wakawatokea, wakazungumza na Yesu. Biblia Habari Njema - BHND Elia na Mose wakawatokea, wakazungumza na Yesu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Elia na Mose wakawatokea, wakazungumza na Yesu. Neno: Bibilia Takatifu Musa na Ilya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Isa. Neno: Maandiko Matakatifu Musa na Ilya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Isa. BIBLIA KISWAHILI Wakatokewa na Eliya pamoja na Musa, nao walikuwa wakizungumza na Yesu. |
Petro akajibu, akamwambia Yesu, Rabi, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya.
Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa ningali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika vitabu vya Manabii na Zaburi.
Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini wengine, Eliya; na wengine kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.
Mnayachunguza maandiko kwa sababu mnadhani kuwa ndani yake ninyi mna uzima wa milele; na maandiko yayo hayo ndiyo yanayonishuhudia.
Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mtumishi mwenzako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.