Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake.
Marko 8:36 - Swahili Revised Union Version Kwa kuwa itamfaidi mtu nini kuupata ulimwengu wote, akiipoteza nafsi yake? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, kuna faida gani mtu kuupata ulimwengu wote na kuyapoteza maisha yake? Biblia Habari Njema - BHND Je, kuna faida gani mtu kuupata ulimwengu wote na kuyapoteza maisha yake? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, kuna faida gani mtu kuupata ulimwengu wote na kuyapoteza maisha yake? Neno: Bibilia Takatifu Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Neno: Maandiko Matakatifu Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa itamfaidi mtu nini kuupata ulimwengu wote, akiipoteza nafsi yake? |
Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake.
Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za BWANA wa majeshi?
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kuipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.
Kwa kuwa inamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akajiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?
Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti.