Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Marko 7:3 - Swahili Revised Union Version

Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Maana Mafarisayo na Wayahudi wengine wote huzingatia mapokeo ya wazee wao: Hawali kitu kabla ya kunawa mikono ipasavyo.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Maana Mafarisayo na Wayahudi wengine wote huzingatia mapokeo ya wazee wao: Hawali kitu kabla ya kunawa mikono ipasavyo.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Maana Mafarisayo na Wayahudi wengine wote huzingatia mapokeo ya wazee wao: hawali kitu kabla ya kunawa mikono ipasavyo.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

(Kwa kuwa Mafarisayo na Wayahudi wote hawali chakula pasipo kunawa kwa kufuata desturi za wazee wao.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa kuwa Mafarisayo na Wayahudi wote hawali chakula pasipo kunawa kwa kufuata desturi za wazee wao.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao;

Tazama sura
Tafsiri zingine



Marko 7:3
10 Marejeleo ya Msalaba  

huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokezana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.


Basi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee, bali hula chakula kwa mikono najisi?


Farisayo huyo alipomwona, alistaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula.


Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kunawa, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.


Nami niliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu.


Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.


Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;