Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Marko 5:41 - Swahili Revised Union Version

Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kisha akamshika mkono, akamwambia, “Talitha, kumi,” maana yake, “Msichana, nakuambia, amka!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kisha akamshika mkono, akamwambia, “Talitha, kumi,” maana yake, “Msichana, nakuambia, amka!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kisha akamshika mkono, akamwambia, “Talitha, kumi,” maana yake, “Msichana, nakuambia, amka!”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Akamshika mtoto mkono, akamwambia, “Talitha koum!” (maana yake, “Msichana, nakuambia: amka!”)

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Akamshika mtoto mkono, akamwambia, “Talitha koum!” (maana yake ni, “Msichana, nakuambia: amka!”)

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Marko 5:41
13 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.


Maana Yeye alisema, na ikawa; Na Yeye aliamuru, ikaumbika.


Akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akaanza kuwatumikia.


Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika.


Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana.


Mara akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu.


(kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.


atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.