Ikiwa kuna njaa katika nchi, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewazingira katika mji wao wowote ule; au ukiwapo msiba wowote, au ugonjwa wowote;
Marko 5:29 - Swahili Revised Union Version Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, akajisikia mwilini mwake kwamba ameponywa ugonjwa wake. Biblia Habari Njema - BHND Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, akajisikia mwilini mwake kwamba ameponywa ugonjwa wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, akajisikia mwilini mwake kwamba ameponywa ugonjwa wake. Neno: Bibilia Takatifu Mara kutoka damu kwake kukakoma, naye akajisikia mwilini mwake amepona kabisa. Neno: Maandiko Matakatifu Mara kutoka damu kwake kukakoma, naye akajisikia mwilini mwake amepona kabisa. BIBLIA KISWAHILI Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule. |
Ikiwa kuna njaa katika nchi, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewazingira katika mji wao wowote ule; au ukiwapo msiba wowote, au ugonjwa wowote;
akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.
Kisha kuhani akiingia ndani kukagua na kuona kuwa pigo halikuenea katika hiyo nyumba baada ya nyumba kupakwa chokaa; ndipo kuhani atatangaza kuwa nyumba hiyo ni safi, maana pigo limepoa.
Tena mwanamume akilala na mwanamke aliye na ugonjwa wake, na kufunua utupu wake; amefunua jito la damu yake, naye mwanamke amefunua jito la damu yake; wote wawili watatengwa mbali na watu wao.
Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake.
Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, nenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.
Na saa ile ile aliwaponya wengi magonjwa yao, na misiba, na pepo wabaya; na vipofu wengi aliwakirimia kuona.