Marko 15:26 - Swahili Revised Union Version Palikuwa na anwani ya mashitaka yake iliyoandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDI. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Na shtaka dhidi yake lilikuwa limeandikwa, “Mfalme wa Wayahudi.” Biblia Habari Njema - BHND Na shtaka dhidi yake lilikuwa limeandikwa, “Mfalme wa Wayahudi.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Na shtaka dhidi yake lilikuwa limeandikwa, “Mfalme wa Wayahudi.” Neno: Bibilia Takatifu Tangazo likaandikwa la mashtaka dhidi yake lenye maneno haya: Mfalme wa Wayahudi. Neno: Maandiko Matakatifu Tangazo likaandikwa la mashtaka dhidi yake lenye maneno haya: “mfalme wa wayahudi.” BIBLIA KISWAHILI Palikuwa na anwani ya mashitaka yake iliyoandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDI. |
Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza popote apendapo.
Lakini hivyo sivyo akusudiavyo mwenyewe, wala sivyo moyo wake uwazavyo; maana katika moyo wake akusudia kuharibu, na kukatilia mbali mataifa, wala si mataifa machache.
nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda.
Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
Wakaweka juu ya kichwa chake mashitaka yake, yaliyoandikwa HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.
Na pamoja naye walisulubisha wanyang'anyi wawili, mmoja mkono wake wa kulia na mmoja mkono wake wa kushoto. [
Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Hata wale waliosulubiwa pamoja naye wakamsuta.
Lakini BWANA, Mungu wako, hakukubali kumsikiza huyo Balaamu; BWANA, Mungu wako, aliyageuza yale maapizo kuwa ni baraka, kwa vile alivyokupenda BWANA, Mungu wako.