Marko 13:36 - Swahili Revised Union Version asije akawasili ghafla akawakuta mmelala. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kesheni ili akija ghafla asije akawakuta mmelala. Biblia Habari Njema - BHND Kesheni ili akija ghafla asije akawakuta mmelala. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kesheni ili akija ghafla asije akawakuta mmelala. Neno: Bibilia Takatifu akija ghafula asije akawakuta mmelala. Neno: Maandiko Matakatifu Kama akija ghafula, asije akawakuta mmelala. BIBLIA KISWAHILI asije akawasili ghafla akawakuta mmelala. |
Nilikuwa nimelala, lakini moyo wangu uko macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.
Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.
Akaja akawakuta wamelala usingizi, akamwambia Petro, Je! Simoni, umelala? Hukuweza kukesha saa moja?
Akaja tena akawakuta wamelala, maana macho yao yamekuwa mazito, wala hawakujua la kumjibu.
Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo;
Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala usingizi kwa huzuni.