Marko 13:33 - Swahili Revised Union Version Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Muwe waangalifu na kesheni, maana hamjui wakati huo utafika lini. Biblia Habari Njema - BHND Muwe waangalifu na kesheni, maana hamjui wakati huo utafika lini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Muwe waangalifu na kesheni, maana hamjui wakati huo utafika lini. Neno: Bibilia Takatifu Jihadharini! Kesheni! Kwa maana hamjui wakati ule utakapowadia. Neno: Maandiko Matakatifu Jihadharini! Kesheni! Kwa maana hamjui wakati ule utakapowadia. BIBLIA KISWAHILI Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo. |
kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.
(Tazama, naja kama mwizi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyobakia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.