Na jeshi lote la mbinguni litafumuliwa, na mbingu zitakunjwa kama karatasi, na jeshi lao lote litanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika.
Marko 13:25 - Swahili Revised Union Version Na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa. Biblia Habari Njema - BHND Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa. Neno: Bibilia Takatifu nazo nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za anga zitatikisika.’ Neno: Maandiko Matakatifu nazo nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za anga zitatikisika.’ BIBLIA KISWAHILI Na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. |
Na jeshi lote la mbinguni litafumuliwa, na mbingu zitakunjwa kama karatasi, na jeshi lao lote litanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika.
Nami nitaonesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi.
Lakini mara tu, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka kutoka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.