Kwa hiyo kinanda changu kimegeuzwa kuwa maombolezo, Na filimbi yangu kuwa sauti yao waliao.
Maombolezo 5:15 - Swahili Revised Union Version Furaha ya mioyo yetu imekoma; Machezo yetu yamegeuka maombolezo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Furaha ya mioyo yetu imetoweka, ngoma zetu zimegeuzwa kuwa ombolezo. Biblia Habari Njema - BHND Furaha ya mioyo yetu imetoweka, ngoma zetu zimegeuzwa kuwa ombolezo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Furaha ya mioyo yetu imetoweka, ngoma zetu zimegeuzwa kuwa ombolezo. Neno: Bibilia Takatifu Furaha imeondoka mioyoni mwetu, kucheza kwetu kumegeuka maombolezo. Neno: Maandiko Matakatifu Furaha imeondoka mioyoni mwetu, kucheza kwetu kumegeuka maombolezo. BIBLIA KISWAHILI Furaha ya mioyo yetu imekoma; Machezo yetu yamegeuka maombolezo. |
Kwa hiyo kinanda changu kimegeuzwa kuwa maombolezo, Na filimbi yangu kuwa sauti yao waliao.
Tena, nitawaondolea sauti ya kicheko, na sauti ya furaha, sauti ya bwana arusi, na sauti ya bibi arusi, sauti ya mawe ya kusagia, na nuru ya mishumaa.
Nami nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa vilio; nami nitatia nguo za magunia katika viuno vyote, na upara katika kila kichwa; nami nitayafanya haya kuwa kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu.