Wala BWANA hakusema ya kwamba atalifuta jina la Israeli litoke chini ya mbingu; lakini akawaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi.
Maombolezo 3:66 - Swahili Revised Union Version Utawafuatia kwa hasira, na kuwaangamiza Wasiwe tena chini ya mbingu za BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uwafuatie kwa hasira, uwaangamize, uwafanye watoweke ulimwenguni.” Biblia Habari Njema - BHND Uwafuatie kwa hasira, uwaangamize, uwafanye watoweke ulimwenguni.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uwafuatie kwa hasira, uwaangamize, uwafanye watoweke ulimwenguni.” Neno: Bibilia Takatifu Wafuatilie katika hasira na uwaangamize chini ya mbingu za Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Wafuatilie katika hasira na uwaangamize kutoka chini ya mbingu za bwana. BIBLIA KISWAHILI Utawafuatia kwa hasira, na kuwaangamiza Wasiwe tena chini ya mbingu za BWANA. |
Wala BWANA hakusema ya kwamba atalifuta jina la Israeli litoke chini ya mbingu; lakini akawaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi.
BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?
Mtawaambia hivi, Miungu hiyo isiyofanya mbingu na nchi, hiyo itaangamia katika nchi, nayo itatoweka chini ya mbingu.
Ee BWANA, unajua wewe; unikumbuke, unijie, ukanilipizie kisasi juu yao wanaoniudhi; usiniondoe kwa uvumilivu wako; ujue ya kuwa ni kwa ajili yako nilivyopatikana na matukano.
Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha BWANA, Mungu wako, katika adui zako wote walio kandokando, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.
BWANA hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya BWANA na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na BWANA atalifuta jina lake chini ya mbingu.
Na wafalme wao atakutilia mkononi mwako, nawe utalipoteza jina lao litoke chini ya mbingu; hapana mtu atakayeweza kusimama mbele yako, hata utakapokwisha kuwaangamiza.