Maombolezo 3:48 - Swahili Revised Union Version Jicho langu lachuruzika mito ya machozi Kwa sababu ya kuharibiwa kwa binti zangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Macho yangu yabubujika mito ya machozi kwa sababu ya kuangamizwa kwa watu wangu. Biblia Habari Njema - BHND Macho yangu yabubujika mito ya machozi kwa sababu ya kuangamizwa kwa watu wangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Macho yangu yabubujika mito ya machozi kwa sababu ya kuangamizwa kwa watu wangu. Neno: Bibilia Takatifu Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu, kwa sababu watu wangu wameangamizwa. Neno: Maandiko Matakatifu Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu, kwa sababu watu wangu wameangamizwa. BIBLIA KISWAHILI Jicho langu lachuruzika mito ya machozi Kwa sababu ya kuharibiwa kwa binti zangu. |
Bali kama hamtaki kusikia, roho yangu italia kwa siri, kwa sababu ya kiburi chenu; na jicho langu litalia sana na kutoka machozi mengi, kwa kuwa kundi la BWANA limechukuliwa mateka.
Nawe utawaambia neno hili, Macho yangu na yatiririke machozi, usiku na mchana, wala yasikome; kwa maana bikira, binti ya watu wangu, amevunjika mavunjiko makuu, kwa jeraha lisiloponyeka.
Mtima wangu, mtima wangu! Naumwa katika moyo wangu wa ndani; moyo wangu umefadhaika ndani yangu; siwezi kunyamaza; kwa sababu umesikia, Ee nafsi yangu, sauti ya tarumbeta, mshindo wa vita.
Laiti kichwa changu kingekuwa maji, na macho yangu kuwa chemchemi ya machozi, ili nipate kulia mchana na usiku kwa ajili yao waliouawa wa binti ya watu wangu!
na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji.
Mimi ninayalilia mambo hayo; Jicho langu, jicho langu linachuruzika machozi; Kwa kuwa mfariji yuko mbali nami, Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi; Watoto wangu wameachwa peke yao, Kwa sababu huyo adui ameshinda.
Macho yangu yamechoka kwa machozi, Mtima wangu umetaabika; Ini langu linamiminwa juu ya nchi Kwa uharibifu wa binti ya watu wangu; Kwa sababu watoto wachanga na wanyonyao, Huzimia katika mitaa ya mji.
Mioyo yao ilimlilia Bwana; Ee ukuta wa binti Sayuni! Machozi na yachuruzike kama mto Mchana na usiku; Usijipatie kupumzika; Mboni ya jicho lako isikome.