Mambo haya mawili yamekupata; Ni nani awezaye kukusikitikia? Ukiwa na uharibifu, na njaa na upanga; Niwezeje kukutuliza?
Maombolezo 3:47 - Swahili Revised Union Version Hofu imetujilia na shimo, Ukiwa na uharibifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kitisho na hofu vimetuandama, tumepatwa na maafa na maangamizi. Biblia Habari Njema - BHND Kitisho na hofu vimetuandama, tumepatwa na maafa na maangamizi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kitisho na hofu vimetuandama, tumepatwa na maafa na maangamizi. Neno: Bibilia Takatifu Tumeteseka kwa hofu kuu na shida ya ghafula, uharibifu na maangamizi.” Neno: Maandiko Matakatifu Tumeteseka kwa hofu kuu na shida ya ghafula, uharibifu na maangamizi.” BIBLIA KISWAHILI Hofu imetujilia na shimo, Ukiwa na uharibifu. |
Mambo haya mawili yamekupata; Ni nani awezaye kukusikitikia? Ukiwa na uharibifu, na njaa na upanga; Niwezeje kukutuliza?
Toka juu amepeleka moto mifupani mwangu, Nao umeishinda; Ametandika wavu aninase miguu, Amenirudisha nyuma; Amenifanya kuwa mtu wa pekee, Na mgonjwa mchana kutwa.
Njia za Sayuni zaomboleza, Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu; Malango yake yote yamekuwa ukiwa, Makuhani wake hupiga kite; Wanawali wake wanahuzunika; Na yeye mwenyewe huona uchungu.