Hata alipokuwa katika taabu, akamsihi BWANA, Mungu wake, akajinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake.
Maombolezo 3:29 - Swahili Revised Union Version Na atie kinywa chake mavumbini; Ikiwa yamkini liko tumaini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yampasa kuinama na kujinyenyekesha, huenda ikawa tumaini bado lipo. Biblia Habari Njema - BHND Yampasa kuinama na kujinyenyekesha, huenda ikawa tumaini bado lipo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yampasa kuinama na kujinyenyekesha, huenda ikawa tumaini bado lipo. Neno: Bibilia Takatifu Hata azike uso wake mavumbini bado tumaini litakuwepo. Neno: Maandiko Matakatifu Na azike uso wake mavumbini bado panawezekana kuwa na matumaini. BIBLIA KISWAHILI Na atie kinywa chake mavumbini; Ikiwa yamkini liko tumaini. |
Hata alipokuwa katika taabu, akamsihi BWANA, Mungu wake, akajinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake.
Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho, asema BWANA; na watoto wako watarejea hata mpaka wao wenyewe.
upate kukumbuka, na kufadhaika, usifumbue kinywa chako tena, kwa sababu ya aibu yako; hapo nitakapokusamehe yote uliyoyatenda, asema Bwana MUNGU.
Ni nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa BWANA, Mungu wenu?
Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?
Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BWANA.
Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipigapiga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;