Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na tuanguke katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu.
Maombolezo 3:22 - Swahili Revised Union Version Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi, huruma zake hazina mwisho. Biblia Habari Njema - BHND Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi, huruma zake hazina mwisho. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi, huruma zake hazina mwisho. Neno: Bibilia Takatifu Kwa sababu ya upendo mkuu wa Mwenyezi Mungu, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa sababu ya upendo mkuu wa bwana, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe. BIBLIA KISWAHILI Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. |
Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na tuanguke katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu.
Ila kwa rehema zako nyingi hukuwakomesha kabisa, wala kuwaacha; kwa maana wewe u Mungu mwenye neema na rehema.
Lakini Yeye, kwa kuwa anayo rehema, Husamehe uovu wala haangamizi. Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake, Wala haiwashi hasira yake yote.
Nenda, ukatangaze maneno haya kuelekea upande wa kaskazini, ukaseme, Rudi, Ee Israeli mwenye kuasi, asema BWANA; sitakutazama kwa hasira; maana mimi ni mwenye rehema, asema BWANA, sitashika hasira hata milele.
Maana mimi ni pamoja nawe, asema BWANA, nikuokoe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokutawanya, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.
Je! Efraimu siye mwanangu mpendwa? Je! Siye mtoto apendezaye? Maana kila nisemapo neno juu yake, ningali nikimkumbuka sana; kwa sababu hiyo moyo wangu unataabika kwa ajili yake; bila shaka nitamrehemu, asema BWANA.
Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.