Maombolezo 3:15 - Swahili Revised Union Version Amenijaza uchungu, Amenikinaisha kwa pakanga. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amenijaza taabu, akanishibisha uchungu. Biblia Habari Njema - BHND Amenijaza taabu, akanishibisha uchungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amenijaza taabu, akanishibisha uchungu. Neno: Bibilia Takatifu Amenijaza kwa majani machungu na kunishibisha kwa nyongo. Neno: Maandiko Matakatifu Amenijaza kwa majani machungu na kunishibisha kwa nyongo. BIBLIA KISWAHILI Amenijaza uchungu, Amenikinaisha kwa pakanga. |
Basi BWANA wa majeshi asema hivi, kuhusu habari ya manabii, Tazama, nitawalisha pakanga, nitawanywesha maji ya uchungu; kwa kuwa kutoka kwa manabii hao wa Yerusalemu kukufuru kumeingia katika nchi yote.
Nawe utawaambia hivi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoutuma kati yenu.
Njia yako na matendo yako yamekupatia haya; huu ndio uovu wako; kwa maana ni uchungu, hakika unafikia hata moyo wako.
bali wameenda katika ushupavu wa mioyo yao wenyewe, na kuandamana na Mabaali, kama walivyofundishwa na baba zao.
Basi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitawalisha pakanga, naam, watu hawa, nami nitawapa maji yenye sumu wayanywe.
Akawaambia, Msiniite Naomi, niiteni Mara kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana.