Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Maombolezo 3:1 - Swahili Revised Union Version

Mimi ni mtu aliyeona mateso Kwa fimbo ya ghadhabu yake.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mimi ni mtu niliyepata mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake Mungu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mimi ni mtu niliyepata mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake Mungu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mimi ni mtu niliyepata mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake Mungu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mimi ndiye mtu aliyeona mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Mimi ndiye mtu aliyeona mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Mimi ni mtu niliyeona mateso Kwa fimbo ya ghadhabu yake.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Maombolezo 3:1
12 Marejeleo ya Msalaba  

Nihurumieni, nihurumieni, enyi rafiki zangu, Kwa maana mkono wa Mungu umenigusa.


Siku zangu ni kama kivuli cha jioni, Nami ninanyauka kama majani.


Wewe, uliyetuonesha mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena. Utatupandisha juu tena Kutoka katika vina virefu chini ya nchi.


Ghadhabu yako imenilemea, Umenitesa kwa mawimbi yako yote.


Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.


Basi wakamtwaa Yeremia, wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika ukumbi wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo.


wanaume, na wanawake, na watoto, na binti za mfalme, na kila mtu ambaye Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, amemwacha pamoja na Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, pia na Yeremia, nabii, na Baruku, mwana wa Neria;


Kwa sababu ya maumivu ya binti ya watu wangu nimeumia mimi; nimevaa kaniki; ushangao umenishika.