Na Gehazi akawatangulia, akaiweka ile fimbo juu ya uso wa mtoto; lakini hapakuwa na sauti, wala majibu. Basi akarudi ili kumlaki, akamwambia, akisema, Mtoto hakuamka.
Luka 9:40 - Swahili Revised Union Version Nikawasihi wanafunzi wako wamtoe, wasiweze. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Niliwaomba wanafunzi wako wamfukuze, lakini hawakuweza.” Biblia Habari Njema - BHND Niliwaomba wanafunzi wako wamfukuze, lakini hawakuweza.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Niliwaomba wanafunzi wako wamfukuze, lakini hawakuweza.” Neno: Bibilia Takatifu Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza.” Neno: Maandiko Matakatifu Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza.” BIBLIA KISWAHILI Nikawasihi wanafunzi wako wamtoe, wasiweze. |
Na Gehazi akawatangulia, akaiweka ile fimbo juu ya uso wa mtoto; lakini hapakuwa na sauti, wala majibu. Basi akarudi ili kumlaki, akamwambia, akisema, Mtoto hakuamka.
Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. [
Akawaita wale Kumi na Wawili, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.
Na tazama, pepo humpagaa, naye mara hupiga kelele; tena humtia kifafa, huku anatokwa na povu, wala hamwachi ila kwa shida, akimchubua-chubua.
Yesu akajibu akasema, Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka, nitakaa nanyi na kuwachukulia hata lini? Mlete mwanao hapa.