Hao Kumi na Wawili Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie.
Luka 9:2 - Swahili Revised Union Version Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kuponya wagonjwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Halafu akawatuma waende kuhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. Biblia Habari Njema - BHND Halafu akawatuma waende kuhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Halafu akawatuma waende kuhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. Neno: Bibilia Takatifu kisha akawatuma waende wakahubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. Neno: Maandiko Matakatifu kisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mwenyezi Mungu na kuponya wagonjwa. BIBLIA KISWAHILI Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kuponya wagonjwa. |
Hao Kumi na Wawili Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie.
Kila mtu alisikiapo neno la ufalme bila kulielewa, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.
Tena Habari Njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda katika kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.
Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung'uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia.
Torati na Manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo Habari Njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu.
Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.