Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Luka 16:16 - Swahili Revised Union Version

16 Torati na Manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo Habari Njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 “Sheria na maandishi ya manabii vilikuwako mpaka wakati wa Yohane Mbatizaji. Tangu hapo, ufalme wa Mungu unahubiriwa, na kila mmoja anauingia kwa nguvu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 “Sheria na maandishi ya manabii vilikuwako mpaka wakati wa Yohane Mbatizaji. Tangu hapo, ufalme wa Mungu unahubiriwa, na kila mmoja anauingia kwa nguvu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 “Sheria na maandishi ya manabii vilikuwako mpaka wakati wa Yohane Mbatizaji. Tangu hapo, ufalme wa Mungu unahubiriwa, na kila mmoja anauingia kwa nguvu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 “Torati na Manabii vilihubiriwa hadi kuja kwa Yahya. Tangu wakati huo Injili ya ufalme wa Mungu inahubiriwa, na kila mmoja hujiingiza kwa nguvu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 “Torati na Manabii vilihubiriwa mpaka kuja kwa Yahya. Tangu wakati huo habari njema za Ufalme wa Mwenyezi Mungu zinahubiriwa, na kila mmoja hujiingiza kwa nguvu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Torati na Manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo Habari Njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu.

Tazama sura Nakili




Luka 16:16
21 Marejeleo ya Msalaba  

Na katika kuenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.


Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.


Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.


Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila namna waliyokuwa nayo watu.


Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu,


Lakini akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu asiweze tena kuingia mjini waziwazi; bali alikaa nje mahali pasipokuwa na watu, wakamwendea kutoka kila upande.


Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung'uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia.


waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia.


Abrahamu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.


Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishika hata mtu akifufuka katika wafu.


Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kuponya wagonjwa.


Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.


Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu.


Basi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, Mwaona kwamba hamfai neno lolote; tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake.


Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika lile bwawa, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.]


Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo