Luka 8:48 - Swahili Revised Union Version Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya; nenda zako na amani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda na amani.” Biblia Habari Njema - BHND Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda na amani.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda na amani.” Neno: Bibilia Takatifu Basi Isa akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani.” Neno: Maandiko Matakatifu Basi Isa akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani.” BIBLIA KISWAHILI Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya; nenda zako na amani. |
Basi Musa akaenda na kurejea kwa Yethro mkwewe, na kumwambia, Nipe ruhusa niende, nakusihi, niwarudie hao ndugu zangu walioko Misri, nipate kuwaona kwamba wako hai hata sasa. Yethro akamwambia Musa, Haya, nenda kwa amani.
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, Hadi ailetapo hukumu ikashinda.
Naye Yesu akamwambia yule afisa, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona wakati ule ule.
Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, akiwa amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.
Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, nenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.
Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara moja.
Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena; naye Paulo akamkazia macho na kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa,
Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.
Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa Habari Njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.
Ndipo Eli akajibu, akasema, Nenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.