Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia, Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe.
Luka 4:24 - Swahili Revised Union Version Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii anayekubaliwa katika nchi yake mwenyewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akaendelea kusema, “Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi kijijini mwake. Biblia Habari Njema - BHND Akaendelea kusema, “Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi kijijini mwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akaendelea kusema, “Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi kijijini mwake. Neno: Bibilia Takatifu Isa akasema, “Amin, nawaambia, hakuna nabii anayekubalika katika mji wake mwenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Isa akasema, “Amin, nawaambia, hakuna nabii anayekubalika katika mji wake mwenyewe. BIBLIA KISWAHILI Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii anayekubaliwa katika nchi yake mwenyewe. |
Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia, Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe.
Kwa maana Yesu mwenyewe alishuhudia ya kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe.
Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nilizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihada kubwa kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi;