Ndipo nikakuungamia dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nilisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA, Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
Luka 23:43 - Swahili Revised Union Version Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akamjibu, “Nakuambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi.” Biblia Habari Njema - BHND Yesu akamjibu, “Nakuambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akamjibu, “Nakuambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi.” Neno: Bibilia Takatifu Isa akamjibu, “Amin, nakuambia, leo utakuwa pamoja nami Paradiso.” Neno: Maandiko Matakatifu Isa akamjibu, “Amin, nakuambia, leo hii utakuwa pamoja nami Paradiso.” BIBLIA KISWAHILI Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi. |
Ndipo nikakuungamia dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nilisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA, Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.
Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? Hadumishi hasira yake milele, kwa maana yeye hufurahia rehema.
Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo.
Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.
Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwemo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.
Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana;
Naye, kwa sababu hii, anaweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.