Luka 23:42 - Swahili Revised Union Version Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha akasema, “Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako.” Biblia Habari Njema - BHND Kisha akasema, “Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha akasema, “Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako.” Neno: Bibilia Takatifu Kisha akasema, “Isa, unikumbuke utakapokuja katika ufalme wako.” Neno: Maandiko Matakatifu Kisha akasema, “Isa, unikumbuke utakapokuja katika Ufalme wako.” BIBLIA KISWAHILI Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. |
Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Mtu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu;
Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipigapiga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lolote lisilofaa.
nikiwashuhudia Wayahudi na Wagiriki wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.
Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.
Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.