Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.
Luka 22:10 - Swahili Revised Union Version Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akiwa amebeba mtungi wa maji; mfuateni mkaingie katika nyumba atakayoingia yeye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akawaambia, “Sikilizeni! Mtakapokuwa mnakwenda mjini, mtakutana na mwanamume anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka ndani ya nyumba atakayoingia. Biblia Habari Njema - BHND Akawaambia, “Sikilizeni! Mtakapokuwa mnakwenda mjini, mtakutana na mwanamume anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka ndani ya nyumba atakayoingia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akawaambia, “Sikilizeni! Mtakapokuwa mnakwenda mjini, mtakutana na mwanamume anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka ndani ya nyumba atakayoingia. Neno: Bibilia Takatifu Isa akawaambia, “Tazameni, mtakapokuwa mkiingia mjini, mtakutana na mwanaume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni hadi kwenye nyumba atakayoingia. Neno: Maandiko Matakatifu Isa akawaambia, “Tazameni, mtakapokuwa mkiingia mjini, mtakutana na mwanaume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka kwenye nyumba atakayoingia. BIBLIA KISWAHILI Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akiwa amebeba mtungi wa maji; mfuateni mkaingie katika nyumba atakayoingia yeye. |
Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.
Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Kiko wapi chumba cha wageni, nipate kula Pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu?
Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi niliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nilikuwapo pamoja nanyi.