ndipo agano langu nililolifanya na Daudi, mtumishi wangu, laweza kuvunjika, hata asiwe na mwana wa kumiliki katika kiti chake cha enzi; tena agano langu nililofanya na Walawi makuhani, wahudumu wangu, laweza kuvunjika.
Luka 20:41 - Swahili Revised Union Version Akawaambia, Wasemaje watu kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akawauliza, “Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? Biblia Habari Njema - BHND Yesu akawauliza, “Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akawauliza, “Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? Neno: Bibilia Takatifu Kisha Isa akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Al-Masihi ni Mwana wa Daudi? Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Isa akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Al-Masihi ni Mwana wa Daudi? BIBLIA KISWAHILI Akawaambia, Wasemaje watu kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi? |
ndipo agano langu nililolifanya na Daudi, mtumishi wangu, laweza kuvunjika, hata asiwe na mwana wa kumiliki katika kiti chake cha enzi; tena agano langu nililofanya na Walawi makuhani, wahudumu wangu, laweza kuvunjika.
Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Mwana wa Daudi.
Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi?
Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa wazawa wake atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi;
Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzawa wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.