Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Luka 2:39 - Swahili Revised Union Version

Basi, walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Hao wazazi walipokwisha fanya yote yaliyoamriwa na sheria ya Bwana, walirudi makwao Nazareti, wilayani Galilaya.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Hao wazazi walipokwisha fanya yote yaliyoamriwa na sheria ya Bwana, walirudi makwao Nazareti, wilayani Galilaya.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Hao wazazi walipokwisha fanya yote yaliyoamriwa na sheria ya Bwana, walirudi makwao Nazareti, wilayani Galilaya.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Yusufu na Mariamu walipokuwa wamekamilisha mambo yote yaliyotakiwa na Torati ya Mwenyezi Mungu, walirudi mjini kwao Nasiri huko Galilaya.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Yusufu na Mariamu walipokuwa wamekamilisha mambo yote yaliyotakiwa na Torati ya Mwenyezi Mungu, walirudi mjini kwao Nasiri huko Galilaya.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Basi, walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Luka 2:39
11 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Ndipo akakubali.

Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka katika mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,

Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiishi katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.

Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Yudea mpaka katika mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa ukoo na jamaa ya Daudi;

Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake.

Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.

Akawaambia, Bila shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe.

Neno lolote ninalowaagiza lizingatieni, usilizidishe, wala usilipunguze.