Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji, tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakasikiliza kitabu cha Torati.
Luka 19:48 - Swahili Revised Union Version wasione la kutenda, kwa kuwa watu wote walikuwa wakiandamana naye, wakimsikiliza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema lakini hawakuwa na la kufanya, maana watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini kabisa. Biblia Habari Njema - BHND lakini hawakuwa na la kufanya, maana watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini kabisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza lakini hawakuwa na la kufanya, maana watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini kabisa. Neno: Bibilia Takatifu Lakini hawakupata nafasi kwa sababu watu wote walimfuata wakiyasikiliza maneno yake kwa usikivu mwingi. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini hawakupata nafasi kwa sababu watu wote walimfuata wakiyasikiliza maneno yake kwa usikivu mwingi. BIBLIA KISWAHILI wasione la kutenda, kwa kuwa watu wote walikuwa wakiandamana naye, wakimsikiliza. |
Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji, tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakasikiliza kitabu cha Torati.
Naye akawa akifundisha kila siku hekaluni. Lakini wakuu wa makuhani, na waandishi, na wakuu wa watu walikuwa wakitafuta njia ya kumwangamiza;
Ikawa siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, na kuihubiri Habari Njema, wakuu wa makuhani na waandishi pamoja na wazee walimtokea ghafla;
Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo.