Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang'anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakamwacha akiwa karibu kufa.
Luka 19:28 - Swahili Revised Union Version Na alipokwisha kusema hayo, alitangulia mbele akipanda kwenda Yerusalemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu alisema hayo, kisha akatangulia mbele yao kuelekea Yerusalemu. Biblia Habari Njema - BHND Yesu alisema hayo, kisha akatangulia mbele yao kuelekea Yerusalemu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu alisema hayo, kisha akatangulia mbele yao kuelekea Yerusalemu. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya Isa kusema haya, alitangulia kupanda kwenda Yerusalemu. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya Isa kusema haya, alitangulia kupanda kwenda Yerusalemu. BIBLIA KISWAHILI Na alipokwisha kusema hayo, alitangulia mbele akipanda kwenda Yerusalemu. |
Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang'anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakamwacha akiwa karibu kufa.
Akawachukua wale Kumi na Wawili, akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii yatatimizwa.
Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliuelekeza uso wake kwenda Yerusalemu;
Basi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga alani mwake; je! Kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee?
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.