Luka 18:2 - Swahili Revised Union Version Akasema, Palikuwa na hakimu katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alisema: “Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu. Biblia Habari Njema - BHND Alisema: “Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alisema: “Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu. Neno: Bibilia Takatifu Akawaambia, “Katika mji mmoja palikuwa hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. Neno: Maandiko Matakatifu Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwepo hakimu ambaye hakumwogopa Mwenyezi Mungu wala kumjali mtu. BIBLIA KISWAHILI Akasema, Palikuwa na hakimu katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. |
Njia kuu zimeachwa, msafiri ameikimbia barabara; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu.
Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendeaendea, akisema, Nipatie haki na adui wangu.
Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,
Basi, bwana wa shamba la mizabibu alisema, Nifanyeje? Nitamtuma mwanangu, mpendwa wangu; yamkini watamheshimu yeye.
Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawaheshimu; basi si ni afadhali zaidi kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?