mimi sistahili hata kidogo hizo rehema zote na kweli yote uliyomfanyia mtumwa wako; maana nilivuka mto huo wa Yordani na fimbo yangu tu, na sasa nimekuwa makundi mawili.
Luka 15:19 - Swahili Revised Union Version sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako.’ Biblia Habari Njema - BHND Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako.’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako.’ Neno: Bibilia Takatifu Sistahili tena kuitwa mwanao; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.’ Neno: Maandiko Matakatifu Sistahili tena kuitwa mwanao; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.’ BIBLIA KISWAHILI sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako. |
mimi sistahili hata kidogo hizo rehema zote na kweli yote uliyomfanyia mtumwa wako; maana nilivuka mto huo wa Yordani na fimbo yangu tu, na sasa nimekuwa makundi mawili.
Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu kwingineko; Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kuishi katika hema za uovu.
Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako;
Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa bado mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu.
Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini mbele ya Yesu, akisema, Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.
Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu nililiudhi kanisa la Mungu.