Tena, mtu mwovu atakapoghairi, na kuuacha uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki, ataponya roho yake, nayo itakuwa hai.
Luka 15:1 - Swahili Revised Union Version Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku moja, watozaushuru na wenye dhambi wengi walikwenda kumsikiliza Yesu. Biblia Habari Njema - BHND Siku moja, watozaushuru na wenye dhambi wengi walikwenda kumsikiliza Yesu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku moja, watozaushuru na wenye dhambi wengi walikwenda kumsikiliza Yesu. Neno: Bibilia Takatifu Basi watoza ushuru na wenye dhambi wote walikuwa wanakusanyika ili wapate kumsikiliza Isa. Neno: Maandiko Matakatifu Basi watoza ushuru na wenye dhambi wote walikuwa wanakusanyika ili wapate kumsikiliza Isa. BIBLIA KISWAHILI Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize. |
Tena, mtu mwovu atakapoghairi, na kuuacha uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki, ataponya roho yake, nayo itakuwa hai.
Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mnapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
Na tazama, wako walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.
Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana.
Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;
Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.