Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka.
Luka 12:57 - Swahili Revised Union Version Na mbona ninyi wenyewe kwa nafsi zenu hamwamui yaliyo haki? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Na kwa nini hamwezi kujiamulia wenyewe jambo jema la kufanya? Biblia Habari Njema - BHND “Na kwa nini hamwezi kujiamulia wenyewe jambo jema la kufanya? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Na kwa nini hamwezi kujiamulia wenyewe jambo jema la kufanya? Neno: Bibilia Takatifu “Kwa nini hamwamui wenyewe lililo haki? Neno: Maandiko Matakatifu “Kwa nini hamwamui wenyewe lililo haki? BIBLIA KISWAHILI Na mbona ninyi wenyewe kwa nafsi zenu hamwamui yaliyo haki? |
Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka.
Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.
Wakati imalizapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.
Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.
Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?