Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, Hao wakae nami. Yeye aendaye katika njia kamilifu, Ndiye atakayenitumikia.
Luka 12:43 - Swahili Revised Union Version Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Heri yake mtumishi huyo ikiwa bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. Biblia Habari Njema - BHND Heri yake mtumishi huyo ikiwa bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Heri yake mtumishi huyo ikiwa bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. Neno: Bibilia Takatifu Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. Neno: Maandiko Matakatifu Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. BIBLIA KISWAHILI Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo. |
Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, Hao wakae nami. Yeye aendaye katika njia kamilifu, Ndiye atakayenitumikia.
Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wowote.
Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?
Kwa hiyo, wapenzi, mnapoyangojea mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane mkiwa na amani, bila doa wala dosari mbele yake.