Luka 10:8 - Swahili Revised Union Version Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama mkifika mji fulani na watu wakiwakaribisha, kuleni wanavyowapeni. Biblia Habari Njema - BHND Kama mkifika mji fulani na watu wakiwakaribisha, kuleni wanavyowapeni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama mkifika mji fulani na watu wakiwakaribisha, kuleni wanavyowapeni. Neno: Bibilia Takatifu “Mkienda katika mji na watu wake wakawakaribisha, kuleni chochote kiwekwacho mbele yenu, Neno: Maandiko Matakatifu “Mkienda katika mji na watu wake wakawakaribisha, kuleni chochote kiwekwacho mbele yenu, BIBLIA KISWAHILI Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu; |
Na mji wowote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni,
akawaambia, Yeyote atakayempokea mtoto huyu kwa jina langu anipokea mimi; na yeyote atakayenipokea mimi ampokea yeye aliyenituma. Kwa kuwa aliye mdogo miongoni mwenu nyote huyo ndiye mkubwa.
Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeaye mtu yeyote nimtumaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi; ampokea yeye aliyenituma.
Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuulizauliza, kwa ajili ya dhamiri.
Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.