Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi kulingana na neno hili, bila shaka kwa hao hakuna asubuhi.
Luka 10:26 - Swahili Revised Union Version Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye akamwuliza, “Imeandikwa nini katika sheria? Unaelewaje?” Biblia Habari Njema - BHND Yeye akamwuliza, “Imeandikwa nini katika sheria? Unaelewaje?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye akamwuliza, “Imeandikwa nini katika sheria? Unaelewaje?” Neno: Bibilia Takatifu Isa akamjibu, “Imeandikwaje katika Torati? Kwani unasoma nini humo?” Neno: Maandiko Matakatifu Isa akamjibu, “Imeandikwaje katika Torati? Kwani unasoma nini humo?” BIBLIA KISWAHILI Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? |
Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi kulingana na neno hili, bila shaka kwa hao hakuna asubuhi.
Na tazama, mwanasheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?
Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.
Kwa maana Musa aliandika juu ya haki itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye hiyo ataishi kwa hiyo.
Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;