Luka 1:54 - Swahili Revised Union Version Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; Ili kukumbuka rehema zake; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amemsaidia Israeli mtumishi wake, akikumbuka huruma yake, Biblia Habari Njema - BHND Amemsaidia Israeli mtumishi wake, akikumbuka huruma yake, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amemsaidia Israeli mtumishi wake, akikumbuka huruma yake, Neno: Bibilia Takatifu Amemsaidia mtumishi wake Israeli, kwa kukumbuka ahadi yake ya kumrehemu Neno: Maandiko Matakatifu Amemsaidia mtumishi wake Israeli, kwa kukumbuka ahadi yake ya kumrehemu BIBLIA KISWAHILI Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; Ili kukumbuka rehema zake; |
Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu.
Kumbuka haya, Ee Yakobo; nawe Israeli, maana wewe u mtumishi wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu; Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi.
Je! Efraimu siye mwanangu mpendwa? Je! Siye mtoto apendezaye? Maana kila nisemapo neno juu yake, ningali nikimkumbuka sana; kwa sababu hiyo moyo wangu unataabika kwa ajili yake; bila shaka nitamrehemu, asema BWANA.
BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.
Wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako, na Abrahamu rehema zako, ulizowaapia baba zetu tangu siku za kale.