Luka 1:53 - Swahili Revised Union Version Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wenye njaa amewashibisha mema, matajiri amewaondoa mikono mitupu. Biblia Habari Njema - BHND Wenye njaa amewashibisha mema, matajiri amewaondoa mikono mitupu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wenye njaa amewashibisha mema, matajiri amewaondoa mikono mitupu. Neno: Bibilia Takatifu Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu. Neno: Maandiko Matakatifu Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu. BIBLIA KISWAHILI Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu. |
Wanasimba hutindikiwa, na kuona njaa; Bali wamtafutao BWANA hawapungukiwi kitu chochote kilicho chema.
Nami nitawainulia miche iwe sifa njema, wala hawataangamizwa kwa njaa katika nchi yao tena, wala hawatatukanwa tena na mataifa.
Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba. Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka.
Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.
Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;
Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam, laiti mngemiliki, ili sisi nasi tumiliki pamoja nanyi!
Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Lakini waliokuwa na njaa sasa hawana njaa tena. Naam, huyo aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini aliye na watoto wengi amehuzunika.