Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa kinywa cha Eliya.
Luka 1:45 - Swahili Revised Union Version Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana aliyokuambia.” Biblia Habari Njema - BHND Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana aliyokuambia.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana aliyokuambia.” Neno: Bibilia Takatifu Amebarikiwa yeye aliyeamini kwamba lile Mwenyezi Mungu alilomwambia litatimizwa.” Neno: Maandiko Matakatifu Amebarikiwa yeye aliyeamini kwamba lile Mwenyezi Mungu alilomwambia litatimizwa.” BIBLIA KISWAHILI Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana. |
Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa kinywa cha Eliya.
Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina.
Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.
Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake.
Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.
Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;