naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuyainua makabila ya Yakobo, na kuwarejesha watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.
Luka 1:16 - Swahili Revised Union Version Na wengi katika Waisraeli atawarejesha kwa Bwana Mungu wao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao. Biblia Habari Njema - BHND Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao. Neno: Bibilia Takatifu Naye atawageuza wengi wa Waisraeli warudi kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wao. Neno: Maandiko Matakatifu Naye atawageuza wengi wa wana wa Israeli warudi kwa Bwana Mwenyezi Mungu wao. BIBLIA KISWAHILI Na wengi katika Waisraeli atawarejesha kwa Bwana Mungu wao. |
naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuyainua makabila ya Yakobo, na kuwarejesha watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.
Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.
Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijia katika hekalu lake ghafla; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema BWANA wa majeshi.
Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.
Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye Juu, Kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake;
Akafika katika nchi yote iliyo karibu na Yordani, akihubiri ubatizo wa toba iletayo ondoleo la dhambi,