Isaya 7:7 - Swahili Revised Union Version Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili halitasimama wala halitakuwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Lakini mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Jambo hilo halitafaulu kamwe. Biblia Habari Njema - BHND “Lakini mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Jambo hilo halitafaulu kamwe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Lakini mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Jambo hilo halitafaulu kamwe. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Bwana Mungu Mwenyezi asema hivi: “ ‘Jambo hili halitatendeka, halitatukia, Neno: Maandiko Matakatifu Lakini bwana Mwenyezi asema hivi: “ ‘Jambo hili halitatendeka, halitatokea, BIBLIA KISWAHILI Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili halitasimama wala halitakuwa. |
Na agano lenu mliloagana na mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo.
Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu, nitatia kulabu yangu katika pua yako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha kwa njia ile ile uliyoijia.
Hata ikawa katika siku za Ahazi, mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, mfalme wa Yuda, Resini, mfalme wa Shamu, na Peka, mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, wakapanda wakaenda Yerusalemu ili kupigana nao, lakini hawakuweza kuushinda.
Haya, na tupande ili kupigana na Yuda na kuwasumbua, tukabomoe mahali tupate kuingia, na kummilikisha mfalme ndani yake, huyo mwana wa Tabeeli.
Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.
na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?